9/08/2011
BUNGE KUCHUNGUZA UFISADI UDA
Ndugu Wanahabari, Suala la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA limeibua hisia kali miongoni mwaWabunge, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla. Suala hili limekuwa tata na kuzusha kilaaina ya maneno. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma imeona ipo haja ya msingiya suala hili kuchunguzwa kwa kina na mhimili wa Bunge.Kwa hiyo, imemuandikia barua Spika wa Bunge, ikimuomba aridhie mapendekezo ya wabungewatakaoundakamati ndogo ya Bunge chini ya Kamati hii ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu zaMashirika ya Umma, ili ichunguze sakata zima la uuzwaji wa Shirika la UDA.Uchunguzi huu umependekezwa kufuatia hisia kwamba taratibu za kuuza Shirika hili pamoja namali zake hazikuzingatia Sheria za nchi na hivyo kupelekea Taifa kuwa katika hatari ya kupotezamali.Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Toleo la mwaka 2007, nyongeza ya sita kifungu cha 13(e),Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ina jukumu la kufuatilia
‘Utekelezaji wa Seraya Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma’
na kanuni ya 13(d)
‘kufanya tathmini ya ufanisi waMashirika ya Umma’
. Ili kutekeleza majukumu haya, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Ummaimemuomba Mhe. Spika aridhie kuundwa kwa kamati ndogo ili kufanya uchunguzi wa suala laShirika la UDA.
Hadidu Rejea
Hadidu rejea za Kamati ndogo ya uchunguzi inayopendekezwa ni kama ifuatavyo:i.
Kuchunguza kama katika zoezi la kubinafsisha Shirika la UDA taratibu zote za Sheriazilifuatwa.ii.
Kuchunguza kama Ofisi ya Msajili wa Hazina na Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma(CHC) walitimiza wajibu wao ipasavyo katika zoezi zima la ubinafsishaji wa Shirika laUDA.iii.
Kuchunguza kama Bodi ya Shirika la UDA ilifuata sheria na kanuni katika kuuza hisazilizouzwa za Shirika la UDA na kama walikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo bilakuhusisha wana hisa. Pia kuchunguza nafasi ya Bodi kwa umoja wake na mjumbe mmojammoja wa Bodi katika zoezi zima husika.
iv.
Kuchunguza nafasi (role) ya wana hisa (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali)katika zoezi zima la kuuzwa kwa hisa (unalloted shares) za UDA kwa Kampuni ya SimonGroup.v.
Kuwaita mbele ya Kamati wadau wote wa suala la UDA hususani Bodi ya UDAiliyokuwepo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UDA, Mmiliki wa Kampuni ya Simon Group ltd,Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa CHC, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na mtumwingine yeyote yule itakavyoonekana inafaa.vi.
Kufanya tathmini ya Shirika la UDA katika mazingira ya sasa ya biashara ya usafirishajiJijini Dar es Salaam.vii.
Kutoa Mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuwa na makosakatika zoezi zima la Ubinafsishaji wa Shirika la UDA.viii.
Kupendekeza namna bora ya kuendesha Shirika la UDA.
Ukomo
Kwa kuwa mamlaka nyingine za Uchunguzi zinaendelea na uchunguzi wake, Kamati hiyo yaBunge itajikita katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu tu na haitahusika na suala kama larushwa au Mahesabu ambayo yanashughulikiwa na TAKUKURU na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali.Isipokuwa Kamati inaweza kuhitaji msaada wa Taasisi hizi katika kutimiza wajibu wake wauchunguzi wa kibunge. Bunge, kwa namna yoyote ile, halitazuiwa kuendelea na uchunguzi wakewakati Serikali (Executive) ikitimiza wajibu wake. Izingatiwe kuwa uchunguzi huu pia unahusishaTaasisi za Serikali zenye mamlaka ya masuala ya Ubinafsishaji na utunzaji wa Mali ya Umma(hivyo Serikali pia inachunguzwa).
Muda wa Uchunguzi
Nimependekeza kuwa uchunguzi huu uchukue jumla ya Siku 14 (kumi na nne tu) na kuwasilishataarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na kisha kwa Spika ambayeataelekeza hatua zitakazofuatia.
Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Uchunguzi.
Kwa kuwa Uchunguzi huu unahusisha mambo mengi, nimependekeza kamati hiyo ndogoihusishe Wabunge wengine katika uchunguzi huu badala ya wajumbe wa Kamati ya Mashirikaya Umma peke yake.
Wajumbe wafuatao wanapendekezwa kuunda Kamati ndogo.1.
Mhe. Murtaza Mangungu, Kilwa Kaskazini (Kamati ya POAC) – Mwenyekiti2.
Mhe. Esther Bulaya, Viti Maalum (Kamati ya POAC)3.
Mhe. Amina Mwidau, Viti Maalumu (Kamati ya POAC)4.
Mhe. David Kafulila, Kigoma Kusini (Kamati ya LAAC)5.
Mhe. Angellah Kairuki, Viti Maalumu (Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala)6.
Mhe. Herbert Mtangi, Muheza (Kamati ya Miundombinu)7.
Mhe. John Mnyika, Ubungo (Mwakilishi Wabunge wa Dar es Salaam)Katibu wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Katibu wa Kamati ya Sheria ndogowanapendekezwa kuwa Makatibu wa
Kamati ndogo ya Uchunguzi wa Ubinafsishaji waShirika la UDA.
Ni matarajio yangu na ya wenzangu kuwa Spika wa Bunge, Mhe.Anne Makinda ataridhiakuundwa kwa Kamati hiyo, ili Bunge liweze kuchukua wajibu wake wa kiuchunguzi na wakuisimamia Serikali. Ninaamini, uchunguzi huo ndio utakaokata mzizi wa fitina kuhusu naniamehusika na achukuliwe hatua gani zichukuliwe kwa maslahi ya Wakazi wa Jiji la Dar esSalaam na Taifa zima kwa ujumla.Nashukuru kwa kunisikiliza.
Kabwe Zuberi Zitto (Mbunge)
No comments:
Post a Comment