Wiki tatu zilizopita kondoo mwenye maneno ya kiarabu alizaliwa katika kijiji cha Uduru Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. kuzaliwa kwa kondoo huyo kumefanya kijiji hicho kupata wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali na dini tofauti japo wengi wao wakiwa waumini wa dini ya Kiislamu ili kumshuhudia kondoo huyo.
Kondoo huyo mwenye neno la kiarabu ubavuni mwake upande wa kulia lenye maana ya neno YASINI kwa tafrisi ya Kiswahili alisababisha watu mbalimbali kumimika kijijini hapo kumshuhudia Kondoo huyo wa ajabu na Kiihistoria ndani ya familia yenye kondoo huyo na hata ndani na nje ya wilaya na mkoa.
Akizungumzia na tukio hilo kijiji hapo mmiliki wa Kondoo huyo, Grace Eliumini Massawe (55) alisema kuwa kondoo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kuwa alikuwa na neno hilo ubavuni mwake kutokana na mama wa kondoo huyo, kumficha ndani kwa wiki zote bila kutoka nje.
Aidha alisema kuwa baada ya kuzaliwa kondoo dume mama yake alibadilisha tabia kwani awali alikuwa akila chakula na wanzake nje jambo lililokuwa kinyume baada ya kuzaliwa kwa kondoo huyo ambapo alikuwa tofauti na kondoo wengine ambapo alianza kumlea mwanae ndani bila kumtoa nje.
Pia alipogundua kuwa kondoo ana neno la kiarabu ni baada ya kondoo huyo kutolewa nje na mama yake ambapo Grace alifikiri kuwa ilikuwa ni herufi ‘W’ yenye rangi kama dhahabu iliyofifia . “kadri siku zilipokuwa zikizidi kupita neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi hali iliyopelekea kutafuta msaada ili kuweza kulitambua maana yake halisi kutoka kwa waumini wa dini ya kiislamu” alisema. “Mara baada ya kufika waumini mbalimbali wa madhehebu ya Kiislamu nyumbani hapo waligundua kuwa kondoo huyo dume alikuwa ameandikwa kwa kiarabu neno lenye tafrisi ya Aya ya ‘YASINI’ ”
“Pia waumini hao walinieleza neno hilo ambalo ni muhimu sana katika kitabu kitakatifu cha quran ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho na pia ni moja ya sura muhimu sana ndani ya kitabu hicho kitakatifu” alisisitiza mama huyo.
Katibu wa Baraza la Waislamu mkoa wa Kilimanjaro BAKWATA Sheikh Rashid Mallya, alikiri kufika kumshuhudia kondoo huyo, nakueleza kuwa maandishi yanayosomeka ubavuni mwa kondoo huyo ni sahihi kama yanavyosomeka katika kitatu kitakatifu cha quran.
Sheikh Mallya alisema aya ya maandishi hayo katika kitabu cha quran ni moja ya sura inayoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake. Alisema kuwa hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu, kwasababu kitabu kitakatifu cha qurani kulishushwa mwezi wa ramadhani, hivyo ishara hii katika kipindi cha mfungo mtukufu wa ramadhani ni ishara kubwa.
inaonekana kama maajabu hayaishi duniani.
2 comments:
duniani kuna mambo.
inawezekana ni alama tu za kawaida sema wameamua kucomplicate, wanyama wengi mbona wana hayo mabaka mabaka?
Post a Comment