Siku bibi Cheka kutoka kundi la muziki wa kizazi kipya TMK Family alipofanya mambo makubwa jukwaani huku mashabiki Lukuki wa wakimshuhudia na kumshangilia kwenye ukumbi wa Mlimani City jumamosi ya wiki iliyopita, ambapo kulifanyika hafla kubwa ya kutoa tuzo kwa wanamuziki bora wa mwaka (KILIMANJARO MUSIC AWARD 2012).
Bibi huyu aliyeibuliwa na meneja wa kundi la TMK Mkubwa Fella, alivalia kama vijana wa kileo wakati alipokuwa akiimba wimbo wake wa "Ni Wewe" huku akishirikiana na Mh. Temba na Chege, alivuta hisia za watu wengi ambao walimshangilia na wangine wakipanda jukwaani kumtunza na kucheza naye, ilikuwa ni kelele na mayowe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake bibi huyo, akiigizastaili za vijana wanaoimba muziki wa Hiphop.
Kama anavyokeana jukwaani mmoja wa mameneja wa bendi ya Mapacha Watatu Bw. Dakota akimtunza bibi Cheka wakati walipokuwa akiimba jukwaani.
Msanii Mh. Temba wa kundi la TMK akimpa tafu bibi Cheka wakati alipokuwa akifanya vitu vyake katika jukwaa la Kilimanjaro Music Awrd 2012 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Mmoja wa mashabiki wa Muziki wa Bibi Cheka akicheza naye jukwaani huku akiwa ameshikilia noti ya shilingi elfu kumi tayari kwa kmtunza bibi huyo machachari wa kundi la TMK Family.
Picha kwa Hisani ya Full Shangwe Blog
Picha kwa Hisani ya Full Shangwe Blog
No comments:
Post a Comment