Pages

Wednesday, September 14, 2011

Mtoto Aliye opolewa Chooni Aendelea Vyema Hospitalini

 msichana mmoja anadaiwa kumtumbukiza chooni mtoto mchanga (pichani) muda mfupi baada ya kuzaliwa kisha wasamaria wema kumuopoa akiwa hai.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilichukua nafasi Jumanne ya Septemba 6, mwaka huu, saa  mbili asubuhi katika Mtaa wa Mkwajuni, mkoani Morogoro na kuvuta kundi kubwa la watu waliojazana kwenye  choo cha nyumba hiyo na kumshuhudia mtoto huyo akielea juu ya kinyesi.

 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo,  Mariana Selemani alisema kuwa alipokea taarifa ya kutupwa chooni kwa mtoto huyo naye akaenda kumjulisha mwenyekiti wa mtaa huo, Khadija  Yekeyeke.
Mjumbe huyo alisema baada ya kuopolewa kichanga hicho kikiwa hai, walikikimbiza hospitali ya mkoa.
Alipoulizwa kama alimfahamu mwanamke aliyefanya ukaliti huo, mjumbe huyo alisema: ‘’ Aliyefanya ukatili huo ni msichana mmoja ambaye anaishi Chamwino, alikuwa na mazoea ya kuja kulala kwa rafiki yake kwenye nyumba hiyo hivyo siku ya tukio alfajiri alijifungua na kumtupa mtoto chooni.”

Mjumbe huyo alisema polisi walikwenda kumkamata msichana huyo lakini walipofika walimkosa kwani alitoroka baada ya kupata taarifa kuwa uhalifu alioufanya umegundulika na alikuwa anasakwa ili atiwe mbaroni.

Hata hivyo mtoto huyo anaendelea vizuri katika hospitali ya mkoa wa morogoro idara ya watoto.


:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

4 comments:

Anonymous said...

oooh MY GOD!!! ALIEFANYA KITENDO CHA KINYAMA HIVYO ALAANIWE

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu anawapa watu uzazi wanamdharau nakutaka kuua viumbe vyake,kazi yakuondoa pumzi na kumpa pumzi mwanadamu ni ya mungu peke yake.wewe dada ulietupa huyu mtoto utakuja kujuta sana.

Anonymous said...

kama siku ya mwisho dhambi zetu zitaonyeshwa kama kwenye Tv huyu dada sijui ataficha wapi uso wake.huyo mtoto anaweza kuja kuwa si ajabu hata rais wa Tz

Anonymous said...

huu ni unyama.akamatwe ahukumiwe kifungo cha maisha