Pages

Wednesday, November 30, 2011

PICHA ZA MATUKIO KATIKA AJALI ILIYOSABABISHWA NA MAFURIKO MONDULI

Basi la abiria la Mali ya kampuni ya Lakrome aina ya Fuso namba T946 ARX likiwa na abiria zaidi ya 40 likitoka Karatu kwenda Rombo nalo ni miongoni mwa mwa vyombo vya usafiri vilivyonusurika katika ajali.
Mfanyakazi wa  Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Augustino Masige,
akiendesha gari namba T573 AHW, akitoka Arusha kwenda Musoma ni miongoni mwa watu walionusurika katika maafa hayo baada ya gari lake aina ya Toyota kusombwa na maji eneo hilo.Masige, alisema katika gari hilo alikuwa peke yake na alikuwa safarini kwenda kwao Musoma likizo na alipofika eneo hilo saa 11 alfajiri gari lake lilisombwa na maji.
Alisema hata hivyo jitihada za kulinasua gari hilo katika tope zinaendelea na kazi ikikamilika atarejea Arusha




Wasafiri waliokuwa wakitoka Karatu na Mti wa Mbu wakitoka kuangalia mwili wa marehemu Samweli.

 Lori la mizigo namba T190 AKW likiwa limebeba mitambo ya kutengeneza barabara likitoka Engaruka kwenda Arusha.


:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

No comments: