Pages

Monday, April 23, 2012

MAWAKILI WENGI WAJITOKEZA MAHAKAMANI KISUTU LEO KUMTETEA ELIZABETH MICHAEL -LULU



Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘lulu’ akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
---
Kamishna wa tume ya haki za binadam, Joaquine De - Mello leo amejitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akiambatana na mawakili wengine wa kujitegemea kumtetea msanii ya sinema, Elizabeth Michael aka Lulu.

Akilitaja jopo la mawakili wanaomtetea Lulu, wakili wa kujitegemea Kennedy Fungamtama, alisema kuwa mama De Mello ni miongoni mwa mawakili pamoja na Furgence Masawe na Peter Kibatala. Hata hivyo hawakuongea lolote mahakamani.
Wakili wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kuwa kesi imekuja kutajwa.Hata hivyo, alisema,  upelelezi bado haujakamilika na kwamba anaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Ikapangwa kutajwa tema Mei 7, 2012.

Awali hali ilikuwa mshike mshike kumpitisha Lulu kutoka chumba cha mahabusu kumleta chumba cha mahakama kwa sababu watu walikuwa wengi pamoja na wanahabari waliokuwa wakimuwinda kupata picha yake.

Korido ilikuwa ndogo kutokana na msongamano wa watu.  Lulu alipitishwa akiwa amezungukwa na maaskari magereza bila shaka  kuzuia asiguswe na watu au kumfanya jambo lolote.

Baada ya purukushani hiyo ya nguo kuchanika, aliingizwa mahakamani akilia kwa sauti kutokana na usumbufu alioupata kutokana na mbanano uliokuwepo,  jambo lililolazimisha mlango wachumba cha mahakama kufungwa na watu kusukumwa nje.

Ikamlazimu Hakimu kutoa amri kuwa kesi hiyo iwe inasomwa mapema zaidi na kuwaamuru  maaskari kuwaondoa watu wote ndipo atolewe kurudishwa mahabusu bila usumbufu tena. Alimpa  Pole Lulu kwa usumbufu alioupata.

Baada ya kutoka Kortini Lulu aliyekuwa amejitanda ushungi, alipelekwa kwenye gari na kuondolewa kwa kasi eneo la mahakama hiyo kwa basi  la magereza, akiwa mfungwa pekee kwenye gari ile iliyojaa pia askari magereza waliokuwa wakimlinda.

Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog



:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

No comments: