Pages

Sunday, April 15, 2012

Diamond kidedea Tuzo za Kili Music Award 2012



Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) Nassib Abdul a.k.a Diamond   usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, baada ya kujinyakulia tuzo tatu.“Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo nimeibuka  na tuzo tatu”,alisema.Tuzo hizo ni ( Mtunzi Bora wa nyimbo,tuzo ya video bora ya Mwaka –moyo wangu na tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume.
Msanii Diamond akipokea tuzo yake ya Mtunzi bora wa nyimbo kutoka kwa Meneja wa bia ya Kilimanjaro,Bw.George Kavishe,katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa wanamuziki bora  Kilimanjaro Music Award 2012 zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuria na waalikwa mbalimbali pamoja na wadau wa muziki kutoka ndani ya Tanzania  na nje ya nchi.
Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment,Evans Bukuku akimkabidhi tuzo yake msanii Diamond,ya video bora ya mwaka.
MKali wa hip hop Tanzania,Chid Benz akimkabidhi tuzo nyingine msanii Diamond ya mtumbuizaji bora wa kiume.
 ******
Mwimbaji Nyota wa Bongo Fleva Nassib Abdul a.k.a Diamond usiku wa Aprili 14,2012 ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia tuzo tatu katika tamasha la Utoaji Tuzo za Kili Music Award 2012.

Diamond ambaye mwaka 2010 aliibuka pia kidedea kwa kuzoa tuzo nyingi na mwaka 2011 kumpa nafasi 20% kwa kuzoa tuzo nyingi mwaka huu amenyakua tuzo ya MTUNZI BORA WA MWAKA, MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME na Video yake ya Mawazo ikinyakua tuzo ya VIDEO BORA YA MWAKA.

Mbali na Diamond aliyebahatika kunyakua Tuzo mbili katika tuzo hizo ni msanii mwingine wa Bongo Fleva Suma Lee aliyenyakua tuzo za WIMBO BORA WA AFRO POP ambao alipata kupitia wimbo wa HAKUNAGA na Tuzo ya pili ni ya WIMBO BORA WA MWAKA.
Ambao pia ni HAKUNAGA.

Aidha msanii Chiopukizi wa Bongo Fleva, Omy Dimpoz nae ametamba baada ya kunyakua tuzo ya WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA wa  NAI NAI aliomshirikisha ALI KIBA na pia alitwaa tuzo ya MSANII BORA ANAECHIPUKIA kupitia wimbo wake huo huo wa NAI NAI.

Nae Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani alikuwa katika kundi hilo la wasanii wenye tuzo mbili baada ya kupata tuzo ya WIMBO BORA WA HIP HOP wa  MATHEMATICS na Tuzo ya MSANII BORA WA HIP HOP.

Wasanii na Vikundi vingine ambavyo vilijinyakulia tuzo ni pamoja na  WIMBO BORA WA RAGGAE Ulikuwa ni ARUSHA GOLD wa kundi la WARRIORS FROM EAST huku Tuzo ya WIMBO BORA WA DANCE HALL ukiwa ni MANENO MANENO wa QUEEN DARLIN.

Tuzo ya WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA alienda kwa Ali Kiba kupitia wimbo wake maarufu wa DUSHELELE , Tuzo ya WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI ilikwenda kwa A.T kwa kibao cha VIFUU UTUNDU.

Tunzo nyingine ilikuwa ni ya  WIMBO BORA WA TAARABU aliyonyakua mwana dada wa kikurya anaeimba Taarabu Aisha Mashauzi kupitia wimbo wa NANI KAMA MAMA wa kundi lake la Mashauzi Classic.

Kundi la Twanga Pepeta nalo lilijinyakulia Tuzo ya WIMBO BORA WA KISWAHILI kupitia wimbo wa DUNIA DARAJA huku Tuzo ya WIMBO BORA WA R&B.
Ikienda kwa Ben Paul kwa wimbo wa NUMBER ONE FAN.

Tuzo nyingine katika mfululizo huo wa Kili Music Award 2012 ilikwenda kwakalijo Kitokololo aliyepata Tuzo ya RAPA BORA WA BAND ambapo Tuzo ya WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI ilienda kwa Wimbo wa KIGEUGEU uliyoimbwa nae JAGUAR.

Tuzo zingine ni za MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE iliyoenda kwa KHADIJA KOPA, tuzo ya  MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI ilienda kwa MANEKE.

Tuzo ya HALL OF FAME ilienda kwa TAASISI JKT, Tuzo ya HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI ilienda kwa Mtu mzima KING KIKII na HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI Ilinyakuliwa na Hayati REMMY ONGALA.

Mkonngwe wa uimbaji wa nyimbo za Kibongo Judith Wambura Habash “Lady Jay Dee alinyakua tuzo ya ya MWIMBAJI BORA WA KIKE huku kijana aliyeshika kasi kutoka kundi la THT Barnaba akifunga jahazi hilo kwa kunyakua tuzo ya MWIMBAJI BORA WA KIUME.
Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

No comments: