Ndege ya ATC muda mchache baada ya kupata ajali hiyo mapema leo
Baadhi ya watu mbali mbali wakiwa wanaelekea eneo la ajali kutoa msaada muda mchache baada ya ajali hiyo
Hivi ndivyo Ndege ya ATC inavyo onekana muda mchache ulio pita, hao ni baadhi ya abiria na watu walio fika eneo hilo muda mchache ulio pita
Hivi Ndivyo inavyo onekana kwa Jirani
**************
Na mwandishi wetu maalum
Ndege ya Shirika la ATC ambayo ilikuwa imetoka Dar es salaam na kutua Kigoma salama na Baada ya muda mchache kuanza safari ya kuelekea Tabora ambapo ndio ilikuwa kwa Runway ilishindwa kuruka na kuacha njia yake kuelekea maporini lakini abiria wote wametoka kwenye ndege hiyo wakiwa salama na wamepelekwa hotelini Kigoma wakati ATCL ikifanya mpango wa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam,” alisema Mfutakamba.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo hakueleza chanzo cha ajali hiyo kwa maelezo kwamba uchunguzi bado unaendelea.
Lakini Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kihenya Kihenya alisema chanzo cha ajali hiyo ni ndege kushindwa kuruka na kuacha njia kisha kuingia porini.
Alisema sababu za kushindwa kuruka, zilitokana na matope yaliyokuwa yametapakaa katika eneo hilo la kiwanja kiasi cha kuifanya ipoteze mwelekeo.“Ilivutwa pembeni kutokana na njia ya kurukia kuwa na matope na ndiyo maana ilipoteza mwelekeo wake wa kawaida. Hali hiyo imesababisha bawa moja la upande wa kulia kukatika kabisa, lakini wasafiri wote wametoka salama na hakuna hata mmoja aliyekufa.”

No comments:
Post a Comment