Wafanyakazi wa Bakery wakiwa hawajui chakufanya
Mfanyakazi wa Royal Bakery akilia kwa uchungu
Polisi wakichukua maelezo
Habari zinasema majambazi watano wakiwa na pikipiki mbili na gari moja na silaha,walivamia eneo hilo majira ya saa tatu za usiku.
Imeelezwa kuwa majambazi hayo moja akiwa na silaha aliingia ndani na bastola na kuwalaza wafanyakazi na wateja ambapo kulikuwa na raia wa kigeni walionyang'anywa wallet na kuvuliwa pete zao kisha wakachukua fedha zote za mauzo huku majambazi waliobaki nje wakifyatua risasi na kufunga barabara kwa takribani dakika kumi.
Dada ambaye ni mfanyakazi wa Bakery hiyo aliyekuwa akieleza anasema kuwa yeye alipigwa vibao lakini hakujeruhiwa zaidi. Baada ya tukio hilo majambazi wakatoweka kusikojulikana ndipo difenda ya polisi ikawasili na kuanza kuchukua maelezo kadhaa.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA: JIACHIE BLOG
No comments:
Post a Comment