Pages

Monday, November 28, 2011

Sumu yapulizwa katikati ya onyesho Nyumbani Lounge

Habari na  Cathbert Angelo ; Msanii wa bendi ya Machozi, Mwinyi akiburudisha mduara mida ya saa nane kasoro wakati tukio hili la kusikitisha lilipotokea.
---
Nazungumza kwa masikitiko sana nikiwa kama mmoja ya waathirika wa jambo hili ambalo limetokea usiku wa leo Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa ni majira ya saa nane kasoro usiku leo wakati bendi ya Machozi ikiburudisha ndani ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam ndipo ilipotokea hali ambayo watu wengi hawakuielewa ila wachache ndiyo waliweza kutambua kilichotokea, nilishtuka kuona watu wanatoka ndani wakikimbilia nje huku wakikohoa, wakipiga chafya na kulalamika kifua kubana na koo kuwasha... ndipo muda mfupi baada ya watu kuwa wametoka nje iligundulika kumbe kuna mtu amepulizia sumu kwa lengo la kuharibu onyesho hilo.

Baada ya kuwa watu wametoka nje, milango yote ilifunguliwa na hewa chafu ilitoka nje na watu kuendelea na Burudani kama kawaida.

Kajunason Blog inawapa pole watu wote waliopatwa na mkasa huu na tunakemea kitendo hicho cha kinyama kwa mtu aliyefanya. Pia tunatakiwa kuheshimu biashara za watu na kuacha roho mbaya ambayo imekuwa ikirudisha maendeleo ya watu nyuma ikiwemo ndugu zako wewe ambaye umefanya kitendo hicho.
***Cathbert Angelo***
******************************************
LADY JAY DEE AMBAYE NI MMILIKI WA MGAHAWA HUO NAE ANASEMA HAYA BAADA YA KUPATA TAARIFA HIYO...
''Hata mkisema tusiiongelee lakini kuna wakati inafika vitu vingine havizuiliki kuvizungumzia
Chuki na husda ni tabia ambayo inaweza hata kuondoa uhai wa mtu (Kijicho???)

Usiku wa ijumaa Nyumbani Lounge wakati watu wanaburudika

Aliingia (waliingia) hawa tunaowaita haters
Muziki umekolea katikati akapuliza spray watu wakaanza kukohoa na kutoka nje

Hivi unaenda vipi sehemu ya biashara ya mtu na kuamua kumfanyia huo ubaya?
Binafsi kama sehemu siipendi siwezi kukanyaga
Hii inadhihirisha mtu (watu) waliofanya hivyo
Wanaipenda sana Nyumbani Lounge
Na wangetamani kuwa na kitu kizuri kama hicho
Ila kwa bahati mbaya Mungu hakuwabariki nacho

Sasa wanaamua kupingana na nguvu za Mungu ili kumuharibia mtu aliepewa
Wanasahau kuwa nguvu ya Mungu ni kubwa na akiamua hashindwi jambo

Nimesikitishwa na kushangazwa sana na hii habari nilioipokea asubuhi ya leo

Kama ametumwa, au kama ni nafsi yake basi ajutie

Hatumuombei mabaya ila
Mwenyezi Mungu na amsamehe

Kama nia ili watu waseme Nyumbani Lounge hapafai
Basi Mungu atamuonyesha, kwani ubaya haushindi wema

Watu tunajaribu kujitaftia rizki
Wala sio kwamba tunatengeneza mahela ya hivooo
Lakini watu vijicho tu roho zinawauma
Roho mbaaayaaaaaa!!!
Mnasahau pesa ni makaratasi tu
Hata mpewe hiyo Nyumbani Lounge leo muibebe mgongoni naamini haiwezi kumaliza shida zenu..
Mnawaeza kuwa na shida zingine pia zinawaandama


Whyyyyyyyyyyyyyyyyyyy????????????????
Kwanini wivu jamani kwa vitu vidogo
Tungekuwa na vya Bakhresa si ndio mngetuma majambazi kabisa watumalize
Shame on you pipo

Na kama nia ni habari ifike mahali isambae itafika
Lakini waelewa na wenye mapenzi ya kweli hawatashindwa kuja tena
Tunawaomba radhi watu wote waliokuwepo
Kwa usumbufu wowote uliojitokeza
NB:
Shukrani kwa fans, wapenzi na supporters wote waliotoka nje
Baada ya hali kuwa shwari wakarudi tena ndani kuendelea na burudani
Tupo, Mungu ni wa wote wema, kwa waouvu
Mfanye maovu mkimuomba awasaidie kwa uovu wenu
Tutafanya mema pia tukimuomba

Kila mtu atapewa kwa wakati wake

HATERS:
Katangazeni basi kuwa Nyumbani Lounge hapafai halafu baada ya hapo na nyie mfungue za kwenu tuzione

Imebidi niandike tu huu waraka,Am a song writer jamani na maneno huwa hayaniishi nikianza kuandika naweza kujaza book zima
Happy Sabath Day

***LADY JAY DEE****
************************************
Kutoka MegVictor, jamani hivi tunaelekea wapi? mbona Tanzania imegeuka kuwa nchi ya watu wenye chuki na maendeleo ya watu?kila anaejitahidi kihalali kukimbizana na maisha lazima kuna watu wanaotaka kumdondosha? kwanini chuki hizo tusizigeuze kuwa chachu ya maendeleo yetu nasi tukapigana kufika hapo huyo tunaemuonea kijicho alipo? Shame on you Haters, and i pray that ujulikane ni nani uliefanya hivyo.hujui kwa akili yako finyu kama nukta ya sindano ungeweza kusababisha maafa?what if kungekuwa na watu wenye matatizo ya pumu?
:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

1 comment:

Anonymous said...

mijitu ina roho mbaya?f@@@@*%k you haters