Pages

Wednesday, October 26, 2011

unataka kaburi la familia? ni million tatu tu!!

“Ardhi sio bidhaa ya petroli wala dhahabu kwamba kuna siku itapungua thamani, kila siku inapanda,”
Huyo si Mwingine ila ni wakili Nyaga Mawalla


Alitumia Sh milioni 200 kuwekeza kwenye ardhi ya ekari 214 na kujenga barabara ya zaidi ya kilometa moja ambayo inaenda kwenye eneo ambalo alinunua ili aweke ofisi yake na kubuni matumizi mengine ya ardhi hiyo.
eneo hilo linapendwa na watu wengi na ameamua kukata vipande na kila kipande anakiuza kwa Sh milioni 30.

Katika eneo hilo ambalo kuna viwanja 182, ameamua kuwauzia watu na wale ambao wananunua anawapa maelekezo ya nyumba zinazotakiwa kujengwa kwenye eneo hilo. “Hili ni eneo langu na anayehitaji kuja kujenga hapa ni lazima atekeleza masharti nitakayompa ya ujenzi.”

katika eneo hilo ametenga eneo la makaburi ambayo mtu yeyote anayetaka azikwe humo yeye na familia yake anauziwa kipande ambacho kitakuwa maalumu kuzikwa watu wa familia yake.

“Makaburi yale siyo yale makubwa ya misalaba kama yaliyoko Kinondoni, hapana mimi naamini makaburi ni eneo la kuheshimiwa hivyo mpango wetu tunahitaji kujengwe makaburi kama yale yaliyoko pale Upanga, Dar es Salaam ambayo yana mvuto zaidi,” anasema.

Anasema wametenga hekta mbili kwa ajili ya makaburi hayo katika eneo hilo lakini pia amewasiliana na Klabu ya Lions kwa ajili ya kujenga bustani nzuri ambayo italifanya eneo hilo la makaburi livutie zaidi. “Yule anayehitaji eneo, kila kipande cha kujenga makaburi ya familia yake tunakiuza Sh milioni tatu,” anasema Mawalla na kusema kuwa fedha hizo zinaingia kwenye asasi ya Mawalla Trust ambayo ndiyo itatunza eneo hilo.

Anasema kuna vipande 100 kwa ajili ya ujenzi wa makaburi hayo na kwa bei hiyo ina maana kuwa zitapatikana Sh milioni 300 ambazo ndizo zitaingizwa kwenye mfuko huu.
:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

No comments: