Pages

Friday, September 16, 2011

NIKIFIKIRIA NATAMANI HATA KUKANA URAIA WANGU.

Mwaka jana nilipoteza ndugu yangu, alikuwa bado ni kijana mdogo, he was just 26 for God sake! Nakumbuka tulipigiwa simu ya kumpoteza usiku saa tisa, na alikuwa umbali wa kama kilometa 2 tu kufika nyumbani kwa mama yake mlandizi akitokea Dar es salaam. Marafiki zake waliokuwa nae wanasema kuwa siku hiyo alikuwa amempigia simu mama yake ambae ni mama yangu mkubwa kuwa atakwenda, masikini ya Mungu mdogo wangu hakujua kama alikuwa anakimbilia kifo. he was going to surprise his mom with his new first car Toyota Celica!! umbali wa kama kilometa mbili ili kufika kwao akavamia semi trela iliyokuwa imepaki barabarani na kufariki papo hapo.gari lilikuja kuvutwa na kupelekwa kituo cha police mlandizi na baada ya muda familia ikaambiwa waliondoe!! yule aliekuwa na gari iliyosababisha ajali hakuchukuliwa hatua zozote na badala yake ilisemekana kuwa ndugu yangu alikuwa kwenye mwendo kasi. inaumiza jinsi wanyonge wanavyoonewa, kwanza hakukuwa na alana yoyote barabarani kuonyesha kuwa mbele yake kulikuwa kuna gari imeharibika! ikaenda enda mwisho wa siku maisha yanasonga mbele lakini hasira niliyoibeba that day mpaka leo hii inanifanya kila wakati ninaposikia habari za ajali za namna hii nitake kupasuka.

 nakumbuka mwaka huo huo aliyewahi kuwa mwandishi wa habari kwenye kampuni ya Daily News na HabariLeo Hayati Dominic Mwita nae alipoteza maisha akitokea harusini na gari yake aina ya RAV4 aliingia kwa nyuma semi-trela lenye namba T632 AGH lililokuwa limesimamishwa katikati ya barabara!!!
mwisho wa siku nalo pia lilipita.


hao ni baadhi tu ya watu waliopoteza maisha na ndoto zao , walioacha watoto na wake zao, wazazi wao, watu waliokuwa wanawategemea, nk, nk, nk, kwa ajali ya aina moja, MADEREVA WA MALORI KUPAKI MALORI YAO BARABARANI.
Kilichonifanya nikakumbuka yote haya ni ajali ya kijana wa pikipiki ambae nae alivamia lori na kufariki hapo hapo. 
 mwisho wa siku itakuwa ni uzembe wa marehemu. lori hilo linasemekana kuharibika toka mchana, lakini halikuondolewa, marehemu alipata ajali majira ya saa tatu na nusu usiku.
 mke wa marehemu akilia kwa uchungu

 mwili wa marehemu mtua ambae ni mkazi wa njia panda mbeya ukiwa umefunikwa



kama ada kama kawa, hakuna atakae wajibishwa wala kuwajibika, meli zitaendelea kuzama, mabasi yataendelea kuanguka, malori yataendelea kupaki barabarani, umeme utaendelea kukatwa na si ajabu kuzimwa kabisa, vyakula vyenye sumu vitaendelea kuingizwa,watoto wataendelea kufundishwa kuipa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, na mengineyo, na mengineyo!!! ooh my beautiful Country!!
:) :( ;) :D ;;-) :-/ :x :P :-* =(( :-O X( :7 B-) :-S #:-S 7:) :(( :)) :| /:) =)) O:-) :-B =; :-c :)] ~X( :-h :-t 8-7 I-) 8-| L-) :-a :-$ [-( :O) 8- 2:-P (:| =P~ #-o =D7 :-SS @-) :^o :-w 7:P 2):) X_X :!! \m/ :-q :-bd ^#(^ :ar!

1 comment:

Anonymous said...

a very sad story.Mwenyezi Mungu akusahaulishe na yote.